SITARUHUSU WATU KUCHAFUA JINA LA UHURU TENA – GACHAGUA
Naibu Rais Rigathi Gachagua ameapa kumtetea aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya yoyote ambayo yatadhalilisha urithi na utu wake.
Akizungumza na vituo vya redio na runinga vya Mlima Kenya, jana jumapili Gachagua alisema umefika wakati nchi iache kumlaumu Uhuru kwa kila kinachotokea kwenda mrama.
Gachagua ameongeza kuwa wakenya wanapaswa kumpa Rais mstaafu na familia yake nafasi ya kufurahia amani yao.
Wakati huo huo gachagua ametoa hakikisho kwa Rais huyo wa zamani kwamba atapewa marupurupu yake ya kustaafu kama inavyotakiwa na sheria.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































