#Local News

JAJI MWILU: KESI YA KUTIMULIWA KWA GACHAGUA ITASHUGHULIKIWA KWA MUJIBU WA SHERIA

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu amesema iwapo mchakato wa kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua utarejea tena mahakamani, majaji hao watafuata utaratibu ulioainishwa kwenye katiba.

Mwilu amesema mchakato huo si wa kipekee kwani unafuata mchakato wa Kikatiba na utazingatiwa kama kesi nyingine yoyote.

Matamshi ya Mwilu yanajiri baada ya maombi 29 kuwasilishwa katika Mahakama ya Juu kusitisha mchakato unaoendelea wa kumbandua mamlakani naibu wa rais kujadiliwa katika bunge la Seneti.

Matumaini ya mwisho ya Gachagua kusitisha mchakato huo yalikatizwa Jumatano baada ya benchi ya majaji 3 kukataa ombi lake.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *