ODM YAONGEZA HAMASISHO MASHINANI
Huku mjadala kuhusu mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ukiendelea, vyama vya siasa vinaongeza juhudi za kuimarisha misingi yao na kuimarisha mshikamano wa wanachama nchini.
Chama cha ODM kimeanza mikutano ya mashauriano na wajumbe kutoka kaunti mbalimbali, kikianza na wawakilishi wa Turkana na Nakuru katika makao yake ya Pawa House jijini Nairobi.
Kiongozi wa ODM Oburu Odinga amesema chama kinalenga kupata makubaliano yenye manufaa katika mazungumzo ya ushirikiano na UDA, huku akisisitiza kuwa ODM bado kina nguvu na kinaungwa mkono kote nchini licha ya kuibuka kwa vuguvugu la Linda Mwananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































