GITONGA: WIMBI LA SIFUNA LINAZIDI KUSHIKA KASI
Mwelekeo wa siasa za upinzani unaendelea kubadilika huku viongozi mbalimbali wakianza kutathmini ushawishi wa viongozi wanaojitokeza na vuguvugu jipya linalozidi kuvutia wananchi.
Mwaniaji wa kiti cha eneo bunge la Othaya Antony Gitonga amesema Edwin Sifuna amekuwa sura mpya yenye mvuto na tishio kwa baadhi ya wanasiasa kutokana na kuongezeka kwa umaarufu wake.
Gitonga amesema vuguvugu la Linda Mwananchi linaendelea kuimarika na kusisitiza kuwa ni wazo ambalo haliwezi kupuuzwa katika siasa za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































