#Football #Sports

NEYMAR ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Neymar ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Brazil baada ya kuondolewa kwenye Kombe la Dunia, akisema wakati wake wa kuitumikia nchi yake umefikia mwisho

Akizungumza baada ya klabu yake ya Santos  kuichapa UCV  mabao 4-2 katika mashindano ya Copa Sudamericana, Neymar amesema alitoa kila alichokuwa nacho kwa Brazil na sasa hana nia ya kuendelea na soka la kimataifa

Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil alirejea kwenye kikosi cha Kombe la Dunia baada ya kukaa karibu miaka mitatu bila kuichezea timu ya taifa, lakini alicheza dakika 37 pekee katika michezo miwili kabla ya kuamua kumaliza safari yake ya kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *