TUSKER WAAGA KAGAME CUP MAPEMA
Tusker wameondolewa kwenye mashindano ya CECAFA Kagame Cup baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Rayon Sports mjini Kigali, Rwanda, na kupoteza nafasi ya kutinga hatua ya mtoano wakiwa bado na mchezo mmoja mkononi
Kipigo hicho kilifuatia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Al-Hilal katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi C, na hivyo kuhitimisha matumaini ya Tusker kusonga mbele kwenye mashindano hayo
Kocha Julien Mette alifanya mabadiliko sita katika kikosi chake baada ya mchezo wa kwanza, lakini juhudi hizo hazikutosha kuzuia kuondolewa kwa timu hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































