#Football #Sports

AWUOR AWATAKA WAKENYA KUENDELEA KUIUNGA MKONO STARLETS

Kipa wa Harambee Starlets Lilian Awuor amewataka Wakenya kuendelea kuiunga mkono timu hiyo inapojitayarisha kuvaana na Senegal katika mchezo muhimu wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake utakaochezwa hapo kesho

Kenya ilianza kampeni yake katika Kundi A kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya wenyeji Morocco, matokeo yaliyoweka kikosi cha kocha Beldine Odemba chini ya shinikizo la kutafuta ushindi ili kuendeleza matumaini ya kutinga robo fainali

Awuor, anayekipiga katika klabu ya Farul Constanța nchini Romania, amesema timu imejifunza kutokana na makosa ya mchezo wa kwanza na inaamini inaweza kurejea kwa nguvu dhidi ya Senegal.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *