INGONGA AONYA WANASIASA WANAOCHOCHEA GHASIA
Kauli za kisiasa zinazoweza kuchochea chuki na vurugu zimeanza kuvutia uangalizi mkali wa vyombo vya sheria huku joto la siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 likizidi kupanda.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga ameonya wanasiasa na watu binafsi kuwa hakuna atakayeachwa iwapo atapatikana akichochea chuki, ghasia au kuhatarisha amani ya nchi.
Ingonga amesema wahusika watakabiliwa na mkono wa sheria huku akiwataka viongozi na wafuasi wao kudumisha amani na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga utulivu wa taifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































