#Football #Sports

WAFCON: DOREEN NABWIRE AIPA STARLETS MATUMAINI YA KUFUZU HATUA YA MCHUJO

Aliyekuwa nahodha wa Harambee Starlets Doreen Nabwire amesema ana imani Kenya inaweza kufufua kampeni yake katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na kufuzu hatua ya robo fainali licha ya kuanza mashindano kwa kichapo

Nabwire amesema kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya wenyeji Morocco hakipaswi kuwavunja moyo wachezaji, akiwataka kuelekeza nguvu zao kwenye mechi zilizobaki dhidi ya Senegal na Algeria

Ameeleza kuwa Starlets wana uwezo wa kushinda michezo yote miwili iliyosalia na kuendeleza matumaini ya kutinga hatua ya mtoano iwapo watacheza kwa nidhamu, kujiamini na kutumia vyema nafasi watakazopata.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

WAFCON: DOREEN NABWIRE AIPA STARLETS MATUMAINI YA KUFUZU HATUA YA MCHUJO

TUSKER WAAGA KAGAME CUP MAPEMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *