#Athletics #Sports

FAITH CHEROTICH ATWAA DHAHABU KATIKA MBIO ZA MITA 3000 KATIKA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

Faith Cherotich ameendelea kuthibitisha ubabe wake katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow kwa rekodi mpya ya mashindano ya dakika 9:01.76

Mwingereza Elise Thorner alimaliza wa pili na kujinyakulia medali ya fedha kwa muda wake bora wa dakika 9:05.45, huku bingwa wa Olimpiki wa Uganda Peruth Chemutai akitwaa shaba baada ya kumaliza wa tatu kwa dakika 9:09.96

Mkenya mwingine, Celestine Biwot, alimaliza katika nafasi ya saba huku ushindi huo ukiendeleza ubabe wa Cherotich katika mbio hizo baada ya pia kutwaa ubingwa wa dunia mwaka uliopita.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

FAITH CHEROTICH ATWAA DHAHABU KATIKA MBIO ZA MITA 3000 KATIKA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA

TUSKER WAAGA KAGAME CUP MAPEMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *