#Local News

GAVANA KIMANI WAMATANGI ASEMA HAKI ZAKE ZILIKIUKWA KATIKA UCHUNGUZI UNAOFANYWA DHIDI YAKE

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi amesema haki zake za kikatiba zilikiukwa katika uchunguzi unaofanywa dhidi yake kuhusu madai ya mikutano ya zabuni ya Seneti.

Akijitetea mbele ya Jaji Rose Ougo katika Mahakama Kuu, Wamatangi aliomba Seneti ijumuishwe kama mhusika mwenye maslahi katika kesi inayopinga utaratibu wa uchunguzi unaoendeshwa dhidi yake na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC.

Kupitia kwa wakili wake Jotham Arwa, gavana huyo amesema Seneti ina maslahi ya moja kwa moja katika suala hilo kwa kuwa baadhi ya madai yanayochunguzwa yanahusiana na mikutano inayodaiwa kuongozwa naye alipokuwa seneta.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *