#Local News

MAWAKILI LEMPAA NA GITAHI GICHUKI WAWASILISHA KESI MAHAKAMANI WAKITAKA ADEN DUALE AONDELEWE OFISINI

Mawakili Lempaa Suyianka na Gitahi Gichuki wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu wakitaka Waziri wa Afya Aden Duale kusimamishwa kushikilia ofisi ya serikali mara moja.

Wanasema matamshi aliyodaiwa kutoa Julai 20, 2026, katika mkutano wa hadhara eneo la Lafey, Kaunti ya Mandera, yanakiuka viwango vya kikatiba vinavyotarajiwa kwa viongozi wa umma.

Mahakama inatarajiwa kusikiliza hoja za pande zote kabla ya kutoa uamuzi kuhusu iwapo matamshi hayo yanakidhi viwango vya uongozi na uadilifu vinavyotakiwa kwa maafisa wa serikali chini ya Katiba.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *