SENETA DAN MAANZO ASEMA HAKUNA UWEZEKANO WA KALONZO KUJIUNGA NA SERIKALI YA KENYA KWANZA
Seneta wa Makueni Dan Maanzo amesema hakuna uwezekano wa kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement, Kalonzo Musyoka, kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Maanzo ambaye ni mshirika wa karibu wa Kalonzo amesema hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Kalonzo na Rais William Ruto kuhusu ushirikiano wa kisiasa.
Kauli ya Maanzo inajiri huku mijadala ya kisiasa ikiendelea kuhusu miungano ya vyama mbalimbali vinavyojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































