IEBC YAKANA MADAI YA KUFUTA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA MATOKEO
Wakati mjadala kuhusu marekebisho ya sheria za uchaguzi ukiendelea, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imejitokeza kufafanua baadhi ya taarifa zilizozua wasiwasi kuhusu usimamizi wa uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi wa mwaka 2026 haupendekezi kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya matokeo ya uchaguzi wala kurejesha mfumo wa uchaguzi wa mwaka 2007.
IEBC imesema mswada huo haupendekezi kubadilisha Kifungu cha 44 cha Sheria ya Uchaguzi kinachoruhusu matumizi ya Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Uchaguzi katika usajili wa wapigakura, utambuzi wa wapigakura na utumaji wa matokeo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































