#Local News

RUTO: MAENDELEO NI WAJIBU WA KIKATIBA WA SERIKALI

Katiba ya Kenya haijaweka msingi wa uongozi wa kidemokrasia pekee, bali pia inalenga kujenga taifa lenye ustawi wa kiuchumi na maisha bora kwa wananchi.

Rais William Ruto amesema Katiba ya Kenya inataka serikali kulinda demokrasia, kupanua fursa za maendeleo, kuimarisha utu wa binadamu na kuboresha maisha ya wananchi.

Ruto amesema maendeleo ni wajibu wa kikatiba wa serikali, akisisitiza kuwa mamlaka ya dola yanapaswa kutumika kuleta ustawi na kuongeza fursa kwa wananchi wote.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *