KENYA YAKOSA MEDALI MBIO ZA MITA 5,000 KWA WANAWAKE
Mbio za masafa marefu zinaendelea kuwa changamoto kwa Kenya katika Michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea mjini Glasgow, huku wanariadha wake wakikosa nafasi ya kutwaa medali nyingine.
Wanariadha wa Kenya walikosa medali katika fainali ya mbio za wanawake za mita 5,000, huku Caroline Nyaga akimaliza katika nafasi ya tano kwa muda bora wa msimu wa dakika 14:54.00.
Rebecca Mwangi alimaliza katika nafasi ya 18, huku Rose Davies wa Australia akitwaa medali ya dhahabu kwa kutumia dakika 14:44.53, ikiwa ni dhahabu yake ya pili katika michezo hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































