#Local News

RUTO AZINDUA MAZUNGUMZO YA KITAIFA KUHUSU DIRA MPYA BAADA YA 2030

Huku kipindi cha utekelezaji wa Dira ya Kenya 2030 kikielekea ukingoni, serikali imeanza maandalizi ya kuweka msingi wa mkakati mpya utakaobeba maendeleo ya taifa katika miaka ijayo.

Rais William Ruto amesema ataongoza uzinduzi wa mazungumzo ya kitaifa kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya Kenya baada ya Dira ya 2030 mnamo Agosti 12.

Ruto amewataka wanasiasa kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana ili kufanikisha ajenda ya maendeleo na mageuzi ya taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *