AMBANI: LEOPARDS YALENGA UBINGWA WA LIGI YA FKF 26/27
Kocha wa AFC Leopards Fred Ambani amesema programu kali ya maandalizi ya kabla ya msimu itaiwezesha timu hiyo kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF msimu wa 2026/27.
Ambani amesema wachezaji wanaendelea na kambi ya mazoezi mjini Nakuru, wakipitia mafunzo ya mbinu, utimamu wa mwili na kujenga mshikamano kabla ya kuelekea nchini Tanzania kwa ziara ya wiki mbili ya maandalizi.
Leopards ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Gor Mahia FC msimu uliopita, huku Ambani akisisitiza kuwa kila kipindi cha mazoezi kinalenga kuinua kiwango cha timu ili iweze kutwaa ubingwa msimu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































