#Local News

KALONZO AKANUSHA UWEZEKANO WA KUSHIRIKIANA NA RUTO

Huku juhudi za kuunganisha upinzani zikiongezeka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, viongozi wanaendelea kuweka wazi misimamo yao kuhusu miungano ya kisiasa.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema hatashirikiana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza kuwa watakuwa wapinzani katika kinyang’anyiro hicho.

Kalonzo amesema viongozi wa serikali wamejaribu kumshawishi ajiunge nao kupitia wajumbe mbalimbali, huku akilihimiza vuguvugu la Linda Mwananchi kuendelea kudumisha umoja wa upinzani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *