STARLETS YAJIKUTA KWENYE HATARI YA KUAGA WAFCON BAADA YA KUPIGWA NA SENEGAL
Matumaini ya Harambee Starlets kutinga hatua ya mtoano katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake yamezidi kufifia baada ya matokeo mengine yasiyoridhisha katika hatua ya makundi.
Harambee Starlets imepoteza bao 1-0 dhidi ya Senegal katika mechi ya Kundi A iliyochezwa jijini Rabat, Morocco, licha ya kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili.
Starlets wanasalia mkiani mwa Kundi A bila pointi na sasa watalazimika kuifunga Algeria katika mchezo wao wa mwisho wa makundi huku wakisubiri matokeo ya mechi nyingine yawe kwa manufaa yao ili kufuzu hatua ya mtoano.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































