KENYA YAANDAA MASHINDANO YA DAVIS CUP AFRIKA
Shirikisho la Tenisi nchini limepata haki ya kuandaa mashindano ya Davis Cup Africa Group IV yatakayofanyika mwezi Juni, hatua inayorejesha mashindano makubwa ya tenisi ya bara Afrika katika jiji la Nairobi.
Mashindano hayo ya siku nne yatakutanisha mataifa manane ambayo ni Algeria, Angola, Botswana, Democratic Republic of the Congo, Ghana, Mozambique, Zimbabwe na Kenya, zikishindana kwa mfumo wa mzunguko na hatua ya mtoano, huku nafasi ya kupanda hadi Kundi la Tatu la Afrika mwaka 2027 ikiwa hatarini.
Katika taarifa iliyotolewa, Shirikisho la Tenisi Kenya limesema mafanikio ya kupata zabuni hiyo ni hatua muhimu inayothibitisha kuimarika kwa hadhi ya Kenya kama kitovu cha kuandaa mashindano ya kimataifa ya michezo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































