#Local News

WINNIE ODINGA AHUDHURIA KONGAMANO LA LINDA GROUND

Mbunge wa EALA ambaye pia ni Mwanawe Hayati Raila Odinga amejiunga na mkutano maalum wa Wajumbe wa chama cha ODM huko Jamhuri Grounds wiki chache baada ya kuidhinishwa kama mwakilishi wa Chama cha ODM.

Hatua hiyo imejiri licha ya kuwepo kwa mkutano sambamba wa kundi la Linda Mwananchi katika Ukumbi wa Ufungamano, kundi ambalo amekuwa akihusishwa nalo.

Katika hotuba yake, Winnie amemtambua Daktari Oburu Oginga kama kiongozi wa chama, huku akiepuka siasa za makundi na badala yake kuhimiza kuwepo kwa nafasi za uongozi na ajira kwa vijana.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *