SOFAPAKA YAKABILIWA NA HATARI YA KUSHUKA
Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars, Twahir Muhiddin, amesema Sofapaka FC inahitaji “muujiza” ili kuepuka kushuka daraja katika Ligi Kuu ya FKF.
Muhiddin ameeleza kuwa vita vya kushuka daraja bado viko wazi huku timu kadhaa zikiwa hatarini msimu ukikaribia tamati.
Sofapaka iko mkiani mwa jedwali ikiwa na alama 15, alama 10 nyuma ya Kariobangi Sharks, ikiwa zimesalia mechi tisa pekee, hali inayowapa kibarua kigumu kujiokoa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































