NTSA YAIMARISHA DORIA BARABARANI
Mamlaka ya usalama barabarani NTSA imetangaza kutumia kamera katika maeneo maalum katika juhudi za kuimarisha usalama barabarani msimu huu wa pasaka, huku idadi ya wasafiri ikiripotiwa kuongezeka katika nyingi ya barabara nchini.
Kwa mujibu wa taarifa, maafisa wa trafiki wataimarisha doria barabarani mbali na uwepo wa mashine za kupima kasi ya magari ili kuhakikisha nidhamu miongoni mwa madereva.
NTSA imewataka watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za trafiki kila mara ili kuepusha maafa barabarani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































