#Football #Sports

CHELSEA WALAUMIWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Kocha wa muda wa Chelsea Calum McFarlane amesema utovu wa nidhamu ulikuwa sababu kubwa iliyosababisha timu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao.

Chelsea walimaliza katika nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufungwa mabao 2-1 na Sunderland Katika mechi ambayo, beki wa Ufaransa Wesley Fofana alitolewa nje kwa kadi nyekundu, ikiwa ni kadi nyekundu ya nane kwa Chelsea katika ligi msimu huu.

McFarlane amesema suala hilo limekuwa tatizo kubwa kwa timu katika msimu uliokuwa na changamoto nyingi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *