MGOMO WA WAUGUZI WAINGIA WIKI YA PILI
Huduma za afya zinaendelea kulemazwa katika hospitali za umma huku mgomo wa wauguzi ukiingia wiki ya pili na kuathiri maelfu ya wagonjwa nchini.
Wauguzi wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta wamejiunga na mgomo wa kitaifa unaoongozwa na Chama cha Wauguzi na Wakunga Kenya wakishinikiza utekelezaji wa Mkataba wa Pamoja wa Kazi wa mwaka 2025–2029.
Huduma za uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General zimeathirika, huku wajawazito na wagonjwa wengine wakilazimika kutafuta matibabu katika hospitali za kibinafsi kutokana na kusimamishwa kwa huduma.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































