#Local News

MIGAWANYIKO YAENDELEA KUTIKISA UPINZANI

Dalili za kutofautiana ndani ya upinzani zimeendelea kujitokeza huku viongozi wakitofautiana kuhusu mwelekeo wa muungano na mgombea wa urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kiongozi wa PNU Peter Munya amesema hatamuunga mkono Rigathi Gachagua iwapo atateuliwa kuwa mgombea wa urais wa muungano wa upinzani, akimshutumu kwa kile alichokiita kauli za kibabe na za kuwadharau viongozi wa vyama vidogo.

Kauli hiyo imeongeza mvutano ndani ya upinzani, baada ya Gachagua kudai kuwa vyama vidogo vya kisiasa katika eneo la Mlima Kenya havina uzito wa kisiasa na kuvitaka kujiunga na DCP.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *