#Local News

RAIS RUTO ASIFIA SERIKALI YAKE KWENYE KONGAMANO LA BAADA YA RUWAZA YA 2030

Rais William Ruto amesema Kenya imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya miundombinu ikilinganishwa na mataifa mengine katika ukanda huu, akitaja ujenzi wa barabara za lami, reli ya SGR na Barabara ya Expressway miongoni mwa mafanikio ya serikali yake.

Rais Ruto amekariri  kuwa taifa lina takriban kilomita elfu 20 za barabara za lami, huku baadhi ya barabara zikiwa zimepanuliwa kuwa njia mbili

Aidha ameeleza kuwa huduma ya umeme  imeendelea kusambazwa kwa  maeneo mengi  nchini, akisema idadi ya maeneo  yaliyounganishwa na umeme imefikia milioni 10 na inatarajiwa kufikia milioni 11.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *