RUTO AMSUTA UHURU, ASEMA ANAPANGA KUMNG’OA MADARAKANI
Rais William Ruto amemkosoa tena mtangulizi wake, akimtuhumu kufadhili upinzani katika juhudi za kudhoofisha serikali yake na kumng’oa mamlakani.
Akizungumza na wakazi wa Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, Ruto amesema serikali ya iliyopita haikushughulikia ipasavyo masuala kama makazi ya bei nafuu na huduma ya afya kwa wote wakati wa utawala wake.
Ruto amesema serikali yake inapaswa kuhukumiwa kwa rekodi ya utendakazi, akiwakosoa wapinzani kwa kutumia kauli za kisiasa kama “wantam” na “must go” bila kuwasilisha mpango mbadala wa kuwaongoza Wakenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































