CHIPU YATAWALA AFRIKA BAADA YA USHINDI WA BARTHES TROPHY
Timu ya Kenya ya raga ya vijana chini ya miaka 20, Chipu, imeibuka mabingwa wa Afrika baada ya kuifunga Namibia kwa alama 33-14 katika fainali ya Barthés Trophy nchini Uganda.
Chipu ilifika fainali baada ya kuishinda Zimbabwe 35-21 katika nusu fainali, na kukamilisha kampeni yake kwa ushindi uliothibitisha ubora wa Kenya katika raga ya vijana barani Afrika.
Nahodha wa Simbas, Samuel Asati, amepongeza kikosi hicho kwa kiwango chake, akisema ushindi huo ni ishara ya nguvu na mustakabali mzuri wa raga ya Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































