GOR MAHIA YAWANIA TAJI LA CECAFA KAGAME DHIDI YA RAYON SPORTS
Gor Mahia itashuka dimbani hii leo mjini Kigali, Rwanda, kuikabili Rayon Sports katika fainali ya mashindano ya CECAFA Kagame Cup.
K’Ogalo inalenga kumaliza ukame wa miaka 41 bila kutwaa ubingwa huo, baada ya mara ya mwisho kushinda taji hilo mwaka 1985 ilipoichapa AFC Leopards mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa Sudan.
Ushindi kwa Gor Mahia utairejeshea Kenya ubingwa wa CECAFA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008, wakati Tusker FC ilipoibuka mabingwa kwa kuishinda Uganda Revenue Authority mabao 2-1 nchini Tanzania.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































