#Football #Sports

LUIS ENRIQUE AWEKA LENGO KUU: PSG KUTWAA KILA KOMBE

Kocha wa Paris Saint-Germain Luis Enrique amesema mabingwa hao wa Ulaya wanalenga kutwaa kila taji msimu huu, wakianza harakati hizo dhidi ya Aston Villa katika fainali ya UEFA Super Cup leo.

PSG ilimaliza msimu uliopita kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo, pamoja na ubingwa wa Ligue 1 kwa msimu wa tano mfululizo na mataji mengine ya kimataifa.

Luis Enrique amesema kikosi chake kiko tayari kuanza kampeni mpya kwa nguvu, huku mechi dhidi ya Aston Villa mjini Salzburg ikiwa nafasi yao ya kwanza ya kutwaa taji msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *