#Football #Sports

LIGI KUU YA FKF KUANZA AGOSTI 29

Msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya FKF unatarajiwa kuanza wikendi ya Agosti 29 na 30, ukiwa na jumla ya mechi tisa katika siku ya kwanza ya mashindano.

Mabingwa watetezi Gor Mahia wataanza kampeni yao nyumbani dhidi ya Murang’a Seal, huku AFC Leopards wakiikaribisha Bandari. Nairobi United itakutana na KCB, huku Ulinzi Stars ikicheza na mabingwa wa Kombe la FKF, Tusker, katika uwanja wa Lang’ata Sports Complex.

Timu zilizopanda daraja, 3K FC, Mombasa United na Migori Youth, zitaanza kwa changamoto ngumu dhidi ya Mara Sugar, Kakamega Homeboyz na Kenya Police mtawalia. Gor Mahia pia inakabiliwa na ratiba ngumu mapema kwenye msimu, ikitarajiwa kukutana na APS Bomet, Bandari, Kakamega Homeboyz, KCB na Nairobi United katika mechi zake zinazofuata.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *