OKANGO: UCHAGUZI LAZIMA UWE HURU NA WA HAKI
Uadilifu wa uchaguzi unaendelea kuwa hoja muhimu huku wito ukitolewa kwa wadau kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa kuzingatia misingi ya sheria na demokrasia.
Mshauri wa Masuala ya Mikakati katika afisi ya Waziri wa Biashara ndogo na kati Fred Okango amesema uchaguzi hauwezi kuzingatiwa kuwa huru na wa haki ikiwa utagubikwa na vitendo vya hongo, ufisadi na vitisho.
Okango amesema wadau wa uchaguzi wanapaswa kuhakikisha mchakato mzima unazingatia misingi ya mfumo wa uchaguzi ili kulinda uhalali wa matokeo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































