#Local News

MGOMO WA WAUGUZI WAFIKIA SIKU YA 16, HUDUMA ZA MATIBABU ZALEMAA

Wauguzi na wakunga nchini wameendelea na maandamano katika miji mbalimbali, wakishinikiza serikali na Baraza la Magavana kutekeleza makubaliano ya pamoja ya mwaka 2017 kuhusu mishahara na kuboresha mazingira ya kazi.

Maandamano hayo yaliendelea Nairobi Alhamisi, huku wanachama wa Muungano wa Wauguzi na Wakunga nchini wakitaka makubaliano hayo yaheshimiwe.

Maelfu ya wahudumu wa afya katika kaunti zote 47 wanaendelea kushiriki mgomo huo ambao umeingia siku ya 16, hali ambayo imeathiri huduma katika hospitali za umma, hasa wodi za uzazi na watoto wachanga.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *