NYUTU: KUMNG’OA RUTO SI KAZI RAHISI
Siasa za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 zinaendelea kushika kasi huku viongozi wakitoa tathmini tofauti kuhusu uwezo wa upinzani kuiondoa serikali madarakani.
Seneta Joe Nyutu amesema kumwondoa Rais William Ruto madarakani si jambo rahisi, akisisitiza kuwa upinzani utalazimika kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma hiyo.
Nyutu amemtetea Rigathi Gachagua, akisema hajawadharau viongozi wengine bali amekuwa akihimiza kila mmoja kuongeza juhudi katika maandalizi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































