KESOGON NA CHESAMIS WATWAA UBINGWA WA TAIFA WA VOLIBOLI
Shule ya upili ya Kesogon na Chesamis Boys wametwaa ubingwa wa taifa wa voliboli katika mashindano ya shule za upili yaliyofanyika mjini thika.
Kesogon ilitwaa taji la wasichana kwa mara ya tatu baada ya kuichapa Soweto Academy kwa seti 3-0 za 25-13, 25-10 na 25-18, na kuongeza ubingwa huo baada ya kutwaa mataji ya mwaka 2023 na 2026.
Kocha wa Kesogon John Marani amesema ushindi huo umetokana na mbinu bora za mchezo, huku akieleza kuwa sasa timu hiyo imeelekeza nguvu zake kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Shule za Afrika Mashariki (FEASSSA).
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































