WAKENYA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA KUPITIA MITANDAO
Upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa sasa umerahisishwa zaidi kupitia mfumo wa kidijitali, huku serikali ikilenga kurahisisha huduma hiyo na kuwaondolea Wakenya ulazima wa kusafiri umbali mrefu kutafuta vyeti hivyo,
Mfumo huo unawawezesha wananchi kupata huduma za usajili wa vizazi kwa njia ya mtandao, hatua ambayo inalenga kupunguza muda na gharama zinazotumika kufuatilia huduma hiyo katika ofisi za serikali.
Serikali imesema matumizi ya mfumo wa kidijitali ni sehemu ya juhudi za kuboresha utoaji wa huduma za umma na kuhakikisha Wakenya wanapata huduma muhimu kwa urahisi na kwa wakati.
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































