#uncategorized

MALAWI YATIKISA AFRIKA KWA KUTINGA FAINALI YA WAFCON

Malawi imefanya maajabu katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) baada ya kuifunga Algeria 3-1 mjini Rabat na kufuzu kwa fainali.

Tabitha Chawinga alifunga mabao mawili huku dada yake Temwa Chawinga akiongeza bao moja, na kuwapa Malawi ushindi wa kihistoria licha ya kuwa washiriki waliokuwa hawapewi nafasi kubwa.

Malawi, iliyoshika nafasi ya 153 duniani, ilitumia vyema kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Algeria Morgane Belkhiter, na kufikisha uongozi wa mabao mawili kabla ya mapumziko.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *