#Local News

SERIKALI YAHAMASISHA USHIRIKI WA UMMA KUHUSU DIRA YA 2060

Serikali imezidisha wito kwa wananchi kushiriki katika maandalizi ya mkakati mpya wa maendeleo ya taifa utakaochukua nafasi ya Dira ya 2030.

Naibu Msemaji wa Serikali Mwanaisha Chidzuga amewataka Wakenya kushiriki kikamilifu katika zoezi la kutoa maoni kuhusu Dira ya 2060, akisema kila mwananchi ana nafasi ya kuchangia mustakabali wa maendeleo ya nchi.

Chidzuga amesema ushiriki wa umma utahakikisha Dira ya 2060 inaakisi maoni na matarajio ya wananchi kuhusu hatua inayofuata ya maendeleo ya Kenya baada ya kukamilika kwa Dira ya 2030.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *