#Local News

MAHAKAMA YASITISHA UTUMIZI WA VYETI VYA KIDIJITALI VYA USAJILI WA MAGARI

Mahakama Kuu imeiagiza Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani NTSA kuendelea kutambua vyeti vya usajili wa magari vya karatasi huku ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi inayopinga kuanzishwa kwa vyeti vya kidijitali.

Jaji Patricia Nyaundi Mande ametoa amri hiyo ya muda katika kesi iliyowasilishwa na Javan Onyango na Emmanuel Kiplagat, ambao wamepinga utekelezaji wa mfumo mpya wa kidijitali wa usajili wa umiliki wa magari unaosimamiwa na NTSA.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *