#Business

KAGWE APIGA MARUFUKU UINGIZAJI WA SUKARI KUTOKA NJE

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ametangaza kuwa serikali haitatoa leseni mpya za uingizaji wa sukari, akisema kuwa uzalishaji wa ndani sasa unatosha kukidhi mahitaji ya nchi na kuwalinda wakulima dhidi ya ushindani usio wa haki.

Akizungumza katika jengo la Kilimo, wakati wa mkutano wa mashauriano na wakulima wa miwa, Kagwe amesema marufuku ya kuingiza sukari nchini inaendelea kutekelezwa huku serikali ikielekeza nguvu zake katika kuimarisha sekta ya sukari ya ndani.

Vile vile Waziri amesema Kenya ina akiba ya kutosha ya sukari na hivyo hakuna sababu ya kuruhusu uingizaji wa sukari zaidi nchini. Kagwe amesisitiza kuwa serikali inadhamiria kuwalinda wazalishaji wa ndani wa sukari kwa kuhakikisha kuwa sukari kutoka nje haijazii soko kwa hasara ya wakulima wa ndani.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *