#Local News

RAIS WILLIAM RUTO AAGIZA SHERIA ZA WALINZI KUZINGATIWA

Rais William Ruto ameagiza taasisi zote za serikali kuhakikisha kampuni za ulinzi binafsi zinazingatia sheria kwa kuwalipa maafisa wa usalama mishahara isiyopungua kiwango cha chini kilichowekwa na serikali.

Akizungumza katika mkutano na maelfu ya maafisa wa usalama wa sekta binafsi uliofanyika Ikulu Alhamisi ya leo Rais Ruto amesema baadhi ya kampuni hazijatekeleza nyongeza ya asilimia 15 ya kiwango cha chini cha mshahara iliyotangazwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *