MBUNGE WA NDIA GEORGE KARIUKI AMEZEA MATE NAFASI YA NAIBU RAIS 2027
Mbunge wa Ndia George Kariuki ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Naibu Rais, akisema Kirinyaga inafaa kupewa nafasi hiyo kutokana na eneo lake la kati ya Mlima Kenya Mashariki na Magharibi.
Kariuki amesema nafasi hiyo inaweza kusaidia kuunganisha jamii za Mlima Kenya zinazokabiliwa na tofauti kuhusu atakayemrithi Naibu Rais Kithure Kindiki, akiwataka wakazi wa eneo hilo kumuunga mkono Rais William Ruto.
Mbunge huyo pia amewataka wakazi wa Mlima Kenya kuepuka siasa za migawanyiko na badala yake kuunga mkono serikali ili ikamilishe ajenda za maendeleo zilizoanzishwa na Rais Ruto.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































