#Local News

HUDUMA ZA AFYA ZALEMAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA  KENYATTA

Huduma katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta zimeathirika baada ya wauguzi kuanza mgomo wao hii leo  kufuatia kutofaulu kwa mazungumzo kati ya uongozi wa hospitali na Chama cha Wauguzi na Wakunga nchini, KNUNM.

Wauguzi hao wanadai kucheleweshwa kwa mishahara na makato ya kisheria, uhaba wa wafanyakazi, pamoja na changamoto za ajira na mafao ya pensheni, wakisema malalamishi yao hayajapatiwa ufumbuzi.

Kutokana na mgomo huo, huduma katika hospitali hiyo kubwa ya rufaa nchini zimevurugika huku wagonjwa wakikumbwa na usumbufu, wakati juhudi za kutafuta suluhu kati ya pande husika zikiendelea.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *