#Football #Sports

KAKAMEGA HIGH NA YALA KUTOANA KIJASHO FAINALI YA SOKA YA KSSSA

Mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari nchini yameingia hatua ya mwisho huku timu za Kakamega High na St. Mary’s Yala zikikutana katika fainali ya soka ya wavulana.

Kakamega ilitinga fainali baada ya kuichapa Menengai mabao 2-1, huku St. Mary’s School Yala ikiiondoa Takaba kwa ushindi wa mabao 2-0 katika michezo ya nusu fainali iliyochezwa Thika.

Upande wa wasichana, St. Joseph’s Girls (JOGA) iliishangaza Archbishop Njenga Girls kwa ushindi wa bao 1-0 na kutinga fainali dhidi ya Nyakach Girls, katika mchezo ambao JOGA inalenga kulipiza kisasi baada ya kufungwa mabao 2-0 kwenye hatua ya makundi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *