MOMBASA UNITED KUANZA SAFARI YA LIGI KUU KWA MTIHANI MZITO
Mombasa United itaanza historia yake katika Ligi Kuu ya Kenya dhidi ya Kakamega Homeboyz, huku kocha Abdulhamid Moallin akikabiliwa na mtihani wake wa kwanza wa kuonyesha utayari wa kikosi chake.
Kwa mujibu wa ratiba ya msimu wa 2026/27 iliyotolewa na Shirikisho la Soka Kenya, mechi hiyo itachezwa wikendi ya Agosti 29 na 30, ikiwa ni mwanzo wa safari ya Mombasa United katika ligi ya daraja la juu nchini.
Moallin, aliyesaidia Young Africans kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania msimu uliopita, anatarajiwa kutumia uzoefu huo kuiongoza Mombasa United kuanza vyema na kujihakikishia nafasi katika ligi ya juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































