BEI YA MAFUTA YAPUNGUA DUNIANI, WAKENYA WASUBIRI NAFUU KUTOKA EPRA
Wamiliki wa magari nchini wanasubiri kwa hamu tangazo la EPRA kuhusu bei mpya za mafuta, baada ya kushuka kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la kimataifa.
EPRA inatarajiwa kutangaza bei mpya za juu za rejareja kesho, Agosti 14, huku bei hizo zikianza kutumika kuanzia Agosti 15. Kwa sasa, petroli Nairobi inauzwa kwa Shilingi 214.03 kwa lita, dizeli Shilingi 222.86 na mafuta ya taa Shilingi 191.38.
Wakenya sasa wanatazamia kuona iwapo kushuka kwa bei ya mafuta duniani kutatafsiriwa kuwa nafuu katika vituo vya mafuta nchini, baada ya bei hizo kudumishwa katika mapitio yaliyopita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































