#Basketball #Sports

KPA YALENGA KUENDELEZA UBABE KATIKA LIGI YA VIKAPU

Kocha wa timu ya mpira wa vikapu ya wanawake ya KPA, Samuel Ocholla, ameitaka timu yake kuendeleza kiwango bora kilichoiwezesha kusalia bila kupoteza mchezo katika Ligi Kuu ya Wanawake nchini.

KPA iliichapa Zetech Sparks kwa alama 70 -39 mwishoni mwa wiki iliyopita na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi kwa ushindi kumi na saba katika michezo kumi na saba.

Ocholla aliwapongeza wachezaji wake kwa kufuata mpango wa mchezo kwa nidhamu licha ya mabadiliko ya uwanja yaliyofanyika dakika za mwisho, akisema ana imani wataendeleza matokeo mazuri katika mechi zijazo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KPA YALENGA KUENDELEZA UBABE KATIKA LIGI YA VIKAPU

KCB YAJIPANGA KABEBERI SEVENS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *