#Rugby #Sports

KCB YAJIPANGA KABEBERI SEVENS

Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Mzunguko wa Raga ya Wachezaji Saba nchini, KCB, sasa wameelekeza nguvu zao katika kuboresha nidhamu na kuimarisha ushirikiano wa wachezaji kuelekea mashindano ya Kabeberi Sevens mwishoni mwa wiki hii.

KCB iliondolewa katika robo fainali ya Kombe Kuu la Dala Sevens baada ya kuchapwa alama 14-12 na Kenya Harlequin, ikimaliza mchezo ikiwa na wachezaji watano pekee kufuatia kutolewa kwa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili.

Kocha Andrew Amonde amesema kuingizwa kwa wachezaji wapya katika kikosi kumeathiri maelewano ya kikosi, lakini ana imani ushirikiano huo utaimarika kadri timu inavyoendelea kucheza pamoja.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KCB YAJIPANGA KABEBERI SEVENS

GOR MAHIA YATINGA FAINALI CECAFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *